Mkuu wa KKKT Awataka Wanafunzi wa Theolojia kufahamu Historia ya Kanisa

Mkuu wa KKKT Askofu Dkt. Fredrick Shoo amewataka wanafunzi wa theolojia, uinjilisti na uhudumu usharika wa Chuo cha Theolojia Kidugala kufahamu kwa usahihi habari za umoja wa Kanisa na kuziendeleza katika wakati huu Kanisa linapoadhimisha miaka 60 tangu kuungana kwa Makanisa saba ya Kilutheri Tanganyika mwaka 1963.Mkuu wa Kanisa amesema hayo katika ziara yake akiwa pamoja na baadhi ya maaskofu kwenye Chuo hicho ambacho kipo KKKT-Dayosisi ya Kusini (Njombe) amewataka pia wanafunzi hao kuwa na mchango chanya katika Jamii kwani kiongozi wa dini ni kiongozi wa Jamii na wala si wa dhehebu au dini fulani pekee.