Mratibu wa kitengo cha Bulding a Caring Community (BCC) cha Dayosisi ya Kaskazini kinachowahudumia watoto wenye ulemavu wa akili katika manispaa ya Moshi, Mdiakonia Elirehema Kaaya amewataka watumishi kuwa na ‘team spirit’ katika utendaji wao wa kazi.
Akizunguza na watumishi kwenye kikao chao cha ndani Umoja Hosteli Machi 24, 2022, alisema wakifanya kazi kama timu itawarahisishia utendaji kazi na kuongeza ufanisi katika kazi. “Tutengeneze na kufanya kazi kama timu ili kuhakikisha tunapeleka huduma Bora kwa watoto. Tukiwa na watumishi na timu nzuri hakika watoto hawa watatabasamu na kufurahi na hii itampa Mungu furaha”Alisema Kaaya.
Naye ‘Spiritual Coordinator’ wa BCC Mch. James Nkya amewaasa watumishi hao kuwa watu wa sala kwa kila jambo wanalolifanya. “Kila tunapoanza jambo tuanze kwa sala, maombi yana nguvu na ukiomba kwa Jina la Yesu Mungu atasikiliza maombi yako, tuombee watoto na huduma hii” alihimiza Mchungaji Nkya.
BC C ni huduma inayoshughulika na watoto wenye ulemavu wa akili inayoshughulika na watoto waliopo nyumbani na wale waliopo kwenye vituo katika sharika 8 za manispaa ya Moshi. Katika sharika hizo kuna vituo ambayo vinawatunza watoto hao kuanzia asubuhi hadi jioni wanaporudi nyumbani.
BCC Ilianzishwa kutoa huduma hiyo kwa lengo la kuwasaidia katika matibabu, mazoezi ya mwili na pia kuwasaidia wazazi waweze kupata muda wa kufanya shughuli kutokana na kushindwa kufanya kazi wakiwa wanawahudumia watoto wao.