Jimbo la Forchheim la Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Ujerumani limeahidi kusaidia kuendeleza ujenzi wa jengo lenye bwalo, jiko, ukumbi na madarasa la Chuo cha Ufundi stadi Sawe ( Sawe Vocational Training Centre).
Akizungumza alipotembelea mradi huo Januari 18, 2022 chuoni hapo, msimamizi wa masuala ya Elimu Afrika Dkt. Topf Wolfgang Jimbo la Forchheim Ujerumani amesema kwa kuwa dhamira yao ni kusaidia upatikanaji wa Elimu bora kwa jamii hususani yenye maisha duni wataendeleza ujenzi huo hadi utakapokamilika.
Dkt. Wolfgang amesema lengo lao kubwa ni kusaidia vijana na jamii kwa ujumla kupata Elimu bora itakayowawezesha kuboresha maisha yao kwa sababu vijana wakipata elimu na ujuzi wataweza kujiajiri na hata kutengeneza ajira kwa watu wengine na kuwa msaada katika kuboresha maisha yao na jamii zao.
“Ni furaha kuona jamii ya Sawe inapata elimu bora vijana wanauwezo wa kujifunza mambo mengi na mapya ambayo yanaweza kuwasaidia kujiajiri na kuwa na maisha bora, kazi ni kubwa lakini kwa Moyo wa upendo walionao kwa Wanasawe kwetu na umoja tulionao kazi hii itakuwa nyepesi Alisema Wolfagang.
Jimbo la Furchheim la Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Ujermani ni Jimbo rafiki na Jimbo la Hai la KKKT Dayosisi ya Kaskazini.
Kati hatua nyingine Mkurugenzi wa taasisi ya Hubert and Renate Schwarz Stiftung inayojishughulisha na masuala ya elimu Bw. Hubert Schwarz ameahidi kushirikiana na Dkt. Wolfagang kuendeleza ujenzi wa jengo hilo hadi utakapo kamilika.
“Naungana na rafiki yangu Dkt. Wolfagang kushirikiana kwa pamoja kuendeleza ujenzi wa jengo hili na kuona unakamilika, ni Imani yangu tukiwa watu wenye Umoja na ndugu katika Kristo tutafanikisha kazi hii kwa haraka” Alisema Hubert.
Jengo hilo la gorofa moja litakuwa na bwalo la kisasa, madarasa, ukumbi wa mikutano na jiko la kisasa litakalotumika kufundisha masomo ya mapishi, namna ya kuhudumia wageni chakula na ukarimu.
Mkuu wa Jimbo la Hai la KKKT Dayosisi ya Kaskazini Mch. Biniel Mallya alimshukuru Mkurugenzi wa Hubert and Renate Schwarz kwa kukubali kushiriki katika ujenzi wa jengo hilo
Hofuman anasema ni furaha kwao kuona jamii ya Sawe inapata Elimu Bora, kazi ni kubwa lakini kwa Moyo wa upendo walionao kwa wanasawe wanaona kazi hiyo kuwa ni Rahisi.
Chuo Cha Ufundi Sawe Cha KKKT Dayosisi ya Kaskazini Usharika wa Sawe kinatoa kozi za ufundi seremala, ushonaji, ujasiriamali, uchomeleaji na kozi fupi fupi za ‘Computer’, mapishi na ukarimu.