Semina Karatu

Semina Karatu

“Fungu la kumi likitolewa kwa hiari na furaha kama tunda la Upendo na shukrani kwa Mungu, linafaa sana.” Hayoa ameyasema Askofu Dkt. Erasto N. Kweka wa KKKT Dayosisi ya Kaskazini (Mstaafu) alipokuwa akifundisha Semina ya Uwakili kwa wachungaji, Wainjilisti na wasaidizi wa sharika huduma za jamii (Parish workers) katika sharika za Jimbo la Karatu iliyofanyika katika Usharika wa Karatu Mjini tarehe 1.3.2023.

Askofu Dkt. Kweka alisema Utoaji unaozingatia ahadi na fungu la kumi kwa kufuata utaratibu wa Kanisa letu unafaa na unabaraka.

Katibu wa Idara ya Mipango na Uwakili Dayosisi ya Kaskazni Mch. Andrew Munisi amesema semina hiyo imelenga  kuwajengea uwezo kuhusu uwakili wetu kwa Bwana wachungaji, wainjilisti, parish workers pamoja na makarani wa Sharika zote 15 za Jimbo la Karatu.

Jimbo la Karatu ni sehemu ya majimbo matano ya KKKT Dayosisi ya Kaskazini, lilianzishwa tarehe  Mwezi Septemba 1972. Lina sharika 15 na mitaa 70,