Semina uwakili yafanyika

Mhe. Askofu Dkt. Fredrick Onael Shoo, Mkuu wa Dayosisi ya Kaskazini, Mkuu wa Kanisa na Mwenyekiti wa CCT, amefungua Mafunzo ya siku mbili kuhusu Uwakili na Miradi, Lutheran Uhuru Hotel & Conference Centre.

Askofu Dkt Shoo alisisitiza kuwa ufundishaji wa Uwakili uzingatie misingi ya Kanisa la Kilutheri ambao ni katika Neno, Ahadi ya Ubatizo, Maungamo na Mapatano ya Kanisa.

Aidha, amewataka washiriki kwenda kuwafundisha washarika na jamii kuhusu uwakili wa muda na vipawa, imani na injili, maisha na utoaji. Amesisitiza kuwa utoaji na kilele cha Uwakili akifananisha ng’ombe atoaye maziwa baada ya kulishwa vema na sio kufundishwa jinsi ya kutoa maziwa.

Naye Mhe. Msaidizi wa Askofu, Mch. Deogratius John Msanya aliwasilisha somo kuhusu Misingi ya Washarika na Sharika kujitegemea Kiuchumi, akikaza kuwa huo ni wajibu wa Kanisa.

Naye Katibu wa Elimu Dkt. Estomihi Makyara alifundisha kwamba Takwimu ni msingi wa mipango ya Maendeleo.

Mch. Andrew Munisi akiwakaribisha Washiriki wa Mafunzo hayo, ameeleza kuwa lengo lake ni kuwaandaa waweze kwenda kufundisha katika zote za Dayosisi.

Alisisitiza Sana umuhimu wa familia kufundishwa waweze kuwa na miradi endelevu ya uchumi.