Siku ya Askofu na Diaspora

Siku ya Askofu na Wanadayosisi waliopo safarini (Diaspora) ilifanyika Disemba 27, 2022 Makuru Machame panapojengwa Makao Makuu ya Chuo Cha Kumbukumbu ya Stephano Moshi (SMMUCo). Siku hii hufanyika Kila mwaka na taarifa za mipango na maendeleo ya Dayosisi hutolewa.

Askofu Dkt. Fredrick Shoo, alitoa taarifa ya Dayosisi kuhusu mipango na utekelezaji wa huduma na shughuli mbalimbali za Maendeleo ikiwemo suala la ujenzi wa makao makuu ya chuo cha Kumbukumbu ya Stefano Moshi (SMMUCo.

Aidha aliwashukuru kwa kushiriki shughuli mbalimbali za Kanisa katika Dayosisi na kuwataka kuendelea kuwa na moyo wa kumtumikia Mungu.

“Ninawashukuru Wachungaji, Sharika, Washarika waliopo safarini na marafiki kutoka nje kwa  kujitoa katika ujenzi  wa  Makao Makuu ya (SMMUCo).”Alisema Askofu Dkt. Shoo.

Baadhi ya Wanadayosisi walioko Safarini Wakishiriki katika Mada za Kuisaidia Dayosisi Kuwa na Maendeleo.