Siku ya Bwana ya Pentekoste – Usharika wa Karatu mjini

Neno kuu  katika ibada hiyo lilikuwa “Roho Mtakatifu Nguvu Yetu”

Ibada ya Siku ya Bwana ya Pentekoste ilifanyika katika kanisa la KKKT Dayosisi ya Kaskazini Usharika wa Karatu mjini. Ibada hii ni pamoja na hitimisho la maadhimisho ya Juma la Pentekoste ambalo kidayosisi imeadhimishwa katika Jimbo la Karatu.

Mheshimiwa Baba Askofu Dkt. Fredrick Shoo aliongoza ibada hiyo. Alianza kwa kuwashukuru na kuwapongeza washarika wa Karatu kwa jinsi ambavyo wanaendelea katika imani, inaonesha kuwa na kundi la Yesu Kristo lililo hai.

Aliendelea kuwapongeza kwa namna walivyowapokea watumishi wa Mungu katika Juma la Pentekoste. “Nimeshuhudiwa jinsi ambavyo mmewapokea wahubiri na wapiga tarumbeta na mkaonesha ukarimu mkubwa sana, Mungu awabariki sana” Alisema Askofu Shoo.

Alihubiri akikaza neno la Mungu kutoka katika kitabu cha Zaburi 143:10.  Alisititiza wakristo kuwa na mazoea ya kuomba uongozi wa Roho Mtakatifu katika kila tunalotenda.