Siku ya wanajimbo K/Kati

Disemba 31 Mkuu wa Jimbo la Kilimanjaro Kati la KKKT Dayosisi ya Kaskazini Mch. Javason Mrema alikutana na Wanajimbo waliopo safarini pamoja na wachungaji  wa Jimbo kujadili masuala mbalimbali ya maendeleo ya Jimbo na Kanisa kwa Ujumla. Mkutano huo ulifanyika katika Ukumbi wa Jimbo hilo.

Akitoa taarifa ya mipango ya maendeleo katika Jimbo, Mkuu wa Jimbo Mch. Mrema alisema siku hiyo itakuwa mahususi kila mwaka kukutana na kuweka Mipango ya Maendeleo katika Jimbo” Kila Mwaka tarehe 31 itakuwa siku ya Wanajimbo waliopo safarini na nyumbani kukaa kwa pamoja na kuweka Mipango ya Maendeleo ya Jimbo letu” alisema Mch. Mrema.

Katika miradi ya Jimbo amesema atahakikisha wanaimarisha miradi iliyopo kabla ya Kuanzisha miradi mipya. Kasema jimbo limeandaa mpango mkakati kuweza kukamilisha miradi mbalimbali na huduma ya Injili na udiakonia.

Anasema kwa sasa jimbo lina miradi mikubwa mitatu na kutaja mradi wa jengo la Kitega Uchumi linalojulikana kwa jina la ‘Youth and Community Centre’, Kituo cha maombi cha Kitimbiriu na Kituo cha kutwa cha Watoto Lowasi  ambapo miradi yote bado haijakamilika. Kawasii washarika wote waliopo nje na ndani ya Jimbo kushirikiana kukamilisha miradi hiyo.

Aidha aliwashukuru wachungaji wote wajimbo waliopo kazini na wastaafu kwa kazi kubwa ambazo zimefanyika katika sharika na mitaa yote. Anasema isingewezekana kupiga hatua kama sii kila mmoja kutumia vipawa ambayo Mungu amempa katika kusimamia kazi katika shamba lake.

Kawataka wanajimbo wote kutumika vizuri na kumzalia Mungu Matunda mema.