Sikukuu ya Uimbaji ngazi ya Dayosisi yafanyika

Sikukuu ya Vijana na Uimbaji katika Dayosisi ya Kaskazini imefanyika Oktoba 16, 2022 katika usharika wa Majengo Jimbo la Kilimanjaro Kati likiwa ni jimbo mwenyeji wa sikukuu hiyo.

Neno kuu katika uimbaji huo lilitoka katika kitabu cha Zaburi ya 116:12-13 “Nimrudishie Bwana nini kwa ukarimu wake wote alionitendea? Nitakipokea kikombe cha wokovu na kulitangaza jina la Bwana”

Neno la mahubiri lilifundishwa na Mkuu wa Kanisa na Dayosisi ya Kaskazini Askofu Dkt. Fredrick Onael Shoo kutoka neno kuu la siku hiyo ya Uimbaji.

Katika mahubiri yake, Baba Askofu alihimiza Wakristo wote kumshukuru  Mungu kwa jinsi anavyowalinda wanadamu na kuwakingia hatari nyingi. Alisema kila mwenye uhai atimize wajibu wake katika kumsifu Mungu.

Alisema katika kuadhimisha sikukuu hiyo ya Uimbaji iadhimishwe kwa kutangaza upendo na kutukuza  ukuu wa Mungu kwa wanadamu.

Tunapaswa kufahamu kuwa, tunamtukuza Mungu kwakuwa ametuumba, katukomboa na kutuweka huru kutoka katika minyororo ya dhambi na kuwataka waimbaji kuondoa neno au dhana ya mashindano na badala yake  wasema tunamshukuru na kumtukuza Mungu kwa nyimbo maana ametuweka huru na kututakasa kwa njia ya Damu ya Bwana na Mwokozi wetu Yesu Kristo.

Aidha Baba askofu aliwapongeza na kushukuru kwaya zote zilizoshiriki siku hiyo ya kumwimbia na kumtukuza Mungu kwa nyimbo.

Jumla ya kwaya 18 zilishiriki uimbaji huo kutoka majimbo 5 ya Dayosisi ambayo ni Hai, Siha, Kilimanjaro Mashariki, Kilimanjaro Kati na Karatu.

Matokeo na alama kwenye mabano za namna kwaya zilivyoonyesha ustadi katika kumwimbia Mungu.

Shule za Sekondari Mchanganyiko Agape Seminari nafasi ya kwanza alama (79), Msufini ya 2 (72.3) na Sekondari wavulana ilikuwa shule moja pekee iliyopata alama 73.

Kwaya za vyuo Mchanganyiko nafasi ya kwanza  ilishikwa na Chuo cha Biblia Mwika (82) ikiwa ni kwaya pekee iliyoshiriki.

Kundi la kwaya za vijana katika sharika nafasi ya kwanza ilishikwa na Kingereka (86), ya pili Moshi Pasua (85), ya tatu Endallah (73.7) na ya nne usharika wa Engarenairobi (69).

Kwa kwaya za Mchanganyiko Sharikani nafasi ya kwanza ilishikwa na Lole (82.3), ya pili Kiboriloni (82), ya tatu Lyamungo Kati (80), ya nne Nasai (78.3) na ya tano ilishikwa na Usharika wa Mbulumbulu (76)

Kwaya za Tarumbeta nafasi ya kwanza ilishikwa na Uuwo (85.5), ya pili Sanya Juu (83 ya tatu Moshi Mjini (81) na ya nne kwaya ya Hai Mjini (75)

Wachungaji na waumini wakiangalia kwaya zikiimba kwa ustadi sikukuu ya Uimbaji na Vijana ya Dayosisi Oktoba 16, 2022 Usharika wa Majengo