Synod ya Nebraska watembelea KKKT Dk

Askofu Scott Johnson wa Synod ya Nebraska na ujumbe wa watu 30 wametembelea KKKT Dayosisi ya Kaskazini Januari 24, 2023 kwenye ofisi kuu ya Dayosisi kwenye ziara yao ya kujifunza mambo kadha wa kadha yanayofanyika katika Dayosisi ikiwa ni njia moja wapo ya kujifunza na kuimarisha mahusiano yao yaliyodumu kwa muda mrefu hivi sasa.

Baba Askofu Dkt. Fredrick Onael Shoo, Mkuu wa KKKT na Dayosisi ya Kaskazini akimkaribisha Askofu Johnson na ujumbe wake, alisema mahusiano kati ya Dayosisi ya Kaskazini na Synod ya Nebraska yamekuwa ya baraka na manufaa makubwa kwa pande zote mbili katika kueneza upendo na Ufalme wa Mungu kwa watu wake.

Amewatakia heri katika ziara yao kujifunza baraka mbalimbali Mungu alizotupa na vilevile changamoto mbalimbali zilizomo katika jamii. Alisema mahausiano yaliyopo watayaendeleza na yataendelea kuwa ya baraka kwa pande zote mbili.

Askofu Johnson kwa upande wake alisema, mahusiano haya yanaishi katika maisha ya watu binafsi, taasisi za Kanisa la Kristo n.k. Anasema kupitia mahusiano haya, wameleana na kutiana nguvu kwa ajili ya maisha na utume ndani ya Mwili wa Kristo.

Baba Askofu Dkt. Fredrick Onael Shoo akizungumza na wageni kutoka Synod ya Nebraska Januari 24, 2023 ofisi kuu ya Dayosisi kwenye ziara yao iliyoanza Jan. 23-Febr. 06, 2023 Kulia ni Askofu Scott Johnson wa Synod ya Nebraska