Uzinduzi Kalali, Watumishi Waingizwa Kazini na Kuagwa, Kamusi ya Kimashami yazinduliwa

Usharika wa Kalali umezindua sehemu ya mapumziko ‘retreat Centre’ itakayokuwa na jumla ya nyumba 8. Kati ya hizo nyumba 6 zitatumika kwaajili ya kulala, 1 itakuwa restaurant na nyingine itatumika kwaajili ya Maombi. Mradi huo hadi kukamilika utagharimu zaidi ya Shilingi Milioni 860.

Pia umezinduliwa ukuta unaozunguka  eneo lote la Kanisa na choo cha kisasa. Uzinduzi huo ulifanywa na Mkuu wa Kanisa na Dayosisi ya Kaskazini Baba Askofu Dkt. Fredrick Onael Shoo akishirikiana na Msaidizi wake Mch. Deogratius Msanya, Mkuu wa Jimbo la Hai Mch. Beniel Mally na Mch. Kiongozi wa Usharika Silas Uronu Jumapili ya Januari 9, 2021.

Pia katika Ibada hiyo Mwinjilisti Apansia Mushi na Parishworker Joyce Mushi walibarikiwa. Sambamba na tendo hilo, viongozi wapya wa Usharika waliingizwa kazini na wale waliomaliza muda wao waliagwa.

Kamusi  ya Kimashami yazinduliwa

 Baba Askofu alizindua kitabu cha Misemo na Kamusi ya lugha ya Kiamachame(Kimashami) kilichoandikwa na Mchungaji Belium Swai. Mch. Swai alisema kitabu hicho amekiandika kwa lengo la kurejesha maadili na kudumisha lugha ya Kimashami kwa urithi wa vizazi vijavyo.

Katika neno la Mahubiri Baba Askofu alihimiza watu kukumbuka zaidi siku na maana ya ubatizo kuliko tunavyokumbuka kumbukumbu za kuzaliwa.

Anasema siku ulipo batizwa ni siku ambayo ulizaliwa mara ya pili siku ya kumkiri Yesu kuwa Bwana na mwokozi wa Maisha yetu. Anasema siku ya kubatizwa inapaswa kupewa uzito mkubwa zaidi kwa kuwa ndiyo siku ambayo ulifanywa kuwa mmoja wa Kundi la Yesu.

Mbunge wa Jimbo la Hai Mhe. Saashisha Mafuwe katika salam zake alimpongeza Mkuu wa Kanisa Askofu Dkt.Fredrick Onael Shoo kwa kazi kubwa anayoifanya ya  kulitumikia Kanisa na Taifa. Anasema amekuwa kiongozi jasiri katika kuonya, Kukosa na kushauri.

Pia alitoa pongezi kwa washarika wa Kalali kwa kujitoa katika kazi ya Mungu “Nawapongeza sana kwa kazi kubwa na nzuri endeleeni kuifanya kazi ya Mungu”Alisema Mbunge huyo.

Baba Askofu akiwabariki Mwinjilisti Apansia Mushi(kushoto) na Parishworker Joyce Mushi(Kulia)