Uzinduzi Ujenzi wa Maabara ya Kisasa- KCMC

Katibu Mkuu Wizara ya Afya Prof. Abel Makubi pamoja na Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Askofu Dkt. Fredrick Shoo, wazindua ujenzi wa maabara ya kisasa katika hospitali ya Kilimanjaro Christian Medical Center (KCMC). Hafla hiyo ilifanyika tarehe 08/07/2022. Maabara hiyo ya kisasa itajikita zaidi katika tafiti mbalimbali, vipimo na mafunzo katika hospitali hiyo.

Katibu Mkuu Wizara ya Afya Prof. Abel Makubi akiweka alama mahali ambapo maabara ya kisasa itajengwa.