Vijana Tunzeni Dhamana na Ufahari Wenu

“Vijana wa Yesu mnaoadhimisha FUNGA MWAKA NA YESU mwaka huu niwaombe, niwasihi, mtunze dhamana, mtunze fahari ya ujana wenu muonekane watu wenye moyo safi na watu wa dhamiri njema, watu wa imani isiyo na unafiki. Ni vyema vijana mkaacha yale yote ambayo yanawafanya mkakumbatia unajisi, muanze mwaka 2024 mkiwa na mioyo safi ”

Hayo aliyasema Askofu Dkt. Fredrick Shoo alipokuwa akifungua Tamasha la FUNGA MWAKA NA YESU lililoandaliwa na Dayosisi ya Kaskazini katika viwanja vya Chuo Kikuu cha Ushirika Moshi, Mkoani Kilimanjaro Disemba 30, 2023.

Aliwataka kuacha yale yote ambayo yamewafanya wawe nje ya imani , nje ya dhamiri jema na nje ya matendo yote yasiyompendeza Mungu.