WALIMU WA ELIMU YA AFYA YA MSINGI WAJENGEWA UWEZO

Mhe. Msaidizi wa Askofu wa KKKT Dayosisi ya Kaskazini Mchungaji Deogratius Msanya amefungua semina ya siku 5 ya kuwajengea uwezo Walimu wa Elimu ya Afya ya Msingi kutoka majimbo 5 ya Dayosisi iliyofanyika Kwenye Kituo cha maburudisho cha Masista wa Ushirika wa Neema Sun Marangu retreat Mei 14 2023

Semina hiyo imeandaliwa na Kitengo cha elimu ya Afya ya Msingi cha Dayosisi ya Kaskazini chenye waratibu kutoka majimbo yote ya Dayosisi.

Mratibu wa Elimu ya Afya ya Msingi wa Dayosisi Bibi. Isaria Megiroo, amesema lengo la semina hiyo  ni kuwaelimisha viongozi na walimu afya wa majimbo ya Dayosisi ya Kaskazini, ili waweze kutoa elimu kwa wengine dhidi ya mbinu na namna ya kuzuia na kujikinga na  magonjwa ya kuambukiza na yasiyo ya kuambukiza katika jamii.

Amesema Mfumo huo wa elimu unaojulikana kwa jina la Training of Trainers (TOT) katika Kanisa unazingatia masomo ya kimwili na ya kiroho.

Baadhi ya walimu wa elimu ya afya Msingi wakiwa katika semina walimu wa walimu – Ushirika wa Neema Sun Marangu Retreat Mei 14, 2023