Wanadayosisi Waliosafarini Wakutana na Askofu

Siku ya Askofu na Wanadayosisi waliopo safarini imefanyika Desemba 27 Makuru Machame panapojengwa Makao Makuu ya Chuo Cha Kumbukumbu ya Stephano Moshi (SMMUCo). Siku hii hufanyika Kila Mwaka na taarifa za maendeleo ya Dayosisi na mipango hutolewa.
Baba Askofu alitoa taarifa ya Dayosisi kuhusu mipango na utekelezaji wa huduma na shughuli mbalimbali za Maendeleo. Aliwashukuru kwa kushiriki shughuli mbalimbali za Kanisa katika Dayosisi na huko walipo.