Waratibu Elimu ya Kikristo na Wachungaji wapata Pikipiki

Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania na Askofu wa Dayosisi ya Kaskazini Dkt. Fredrick Onael Shoo, amegawa pikipiki 8 kwa Waratibu wa Elimu ya Kikristo Majimboni na Wachungaji wawili hedikota ya Dayosisi Machi 16,2023.Baba askofu amegawa pikipiki hizo kufuatia utaratibu uliowekwa na Dayosisi kupitia Idara ya Misioni na Uinjilisti ya kuwawezesha Wtumishi kupata pikipiki kwa njia ya uenyeji na kwa bei nafuu.Pikipiki moja inagharimu kiasi cha shilingi milioni mbili na laki sita (2,600,000/=) ikiwa tayari imekatiwa vibali vyote ambapo mnufaika anapewa kwa unafuu wa nusu bei sawa na shilingi milioni moja na laki tatu (1,300,000/=) badala ya milioni mbili na laki sita.Akigawa pikipiki hizo, Baba Askofu Dkt. Shoo alitoa wito kwa watumishi hao kutumia vyombo hivyo kwa uangalifu na kwa ajili ya kufanikisha kazi ya Bwana. Anasema vyombo hivyo ni kwa ajili ya kuwasaidia kuwafikia na kuwahudumia watu kwa haraka na kwa mapana zaidi.“Niwaombe mkavitumie vyombo hivi kwa kazi iliyo kusudiwa na si vinginevyo, hizi ni sadaka za watu mkazitumie kuongeza ufanisi katika kazi” Alisema Askofu Dkt. Shoo.

Baba Askofu Dkt. Fredrick Shoo akibariki pikipiki kabla ya kuzigawa kwa Waratibu wa Elimu ya Kikristo Majimboni na Wachungaji 2, Machi 16, 2023