Warsha Mpango Mkakati Miaka Mitano

Mkuu wa KKKT na Dayosisi ya Kaskazini Askofu Dkt. Fredrick Onael Shoo amefungua warsha ya siku moja ya wakuu wa Idara na Vitengo ndani ya Dayosisi ya Kaskazini iliyofanyika Uhuru Hotel Januari 26, 2022 kuelezea mpango Mkakati wa Kanisa wa miaka mitano 2021/22 hadi 2025/26.

Warsha hiyo ilifanywa na katibu Mkuu wa KKKT Eng. Robert Kitundu, Naibu Katibu Mkuu wa Mipango na Maendeleo Bw. Simon Daffi, na Afisa Usimamizi, Tathmini na Mafunzo Bibi. Pendo-Edina Mahoo.

Mpango Mkakati wa huo wa Kanisa umehusishwa na vipaumbele vya taasisi zingine zenye ushirikiano na KKKT na  mitazamo inayoshabihiana Kitaifa, kibara la Afrika na kimataifa.

Vipaombele hivyo ni vile vilivyomo katika mpango wa tatu wa Serikali ya Tanzania (2021/2022-2025/2026) na mpango wa 6 wa maendeleo wa  Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) wa 2021/2022-2025/2026.