Woongo: Usharika wazinduliwa, watoto wabatizwa

Mhe. Askofu Dkt. Fredrick Onael Shoo, Mkuu wa Dayosisi, KKKT na CCT, ameongoza Ibada leo Disemba 2021 katika Usharika wa Woongo Jimbo la Hai ambapo alizindua Nyumba ya Mchungaji yenye thamani ya Tzs. 375 milioni; alizindua Usharika wa Woongo; alibatiza watoto wadogo; aliwaingiza kazini Mwinjilisti Kantate Mushi na Parishworker Happiness Kimaro; na kutoa Baraka ya Jubilii kwa walitimiza miaka 25, 50 na 75 toka kuzaliwa, kubatizwa, kipaimara na ndoa.

Akizindua Usharika, washarika walikubali kuongezewa madaraka, baraka na wajibu. Washarika waliahidi kutimiza wajibu huo kwa msaada wa Mungu.

Akihubiri Neno la Mungu toka Mika 5:1-5a, aliwatia moyo wafuasi wa Yesu kwamba wasiogope udogo wao wala kudharauliwa kwao; bali wasonge mbele kwa kuwa Yesu atawawezesha kufanya mambo makubwa na kuwapa Amani.

Aliibariki Kamati ya kukusanya fedha kwa ajili ya Ununuzi wa gari la Usharika 2022 na alizindua Kitabu cha Historia ya Usharika wa Woongo toka Injili kuingia na Maendeleo yake.

Aidha, Usharika uliishika mkono familia ya aliyekuwa Mlinzi Bw. Eliezeri Kimaro.