BCC Washiriki Kili marathon

Watoto wenye Ulemavu wa akili katika Sharika za Manispaa ya Moshi wanaotunzwa na kitengo cha Building a caring Community (BCC) cha KKKT Dayosisi ya Kaskazini wameshiriki mbio za Kilimanjaro Marathon zilizofanyika Jumapili ya Februari 27, 2022. Mbio hizo zilianzia katika viwanja vya Chuo cha Ushirika Moshi na kumalizika viwanjani hapo.

Jumla ya watoto 24 wa BCC wamekimbia Umbali wa Km 5. Mhe. Waziri Mkuu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Kassim Majaliwa alizindua rasmi Mashndaano hayo ambapo kwa sasa yametimiza miak 20 tangu kuanzishwa kwake mwaka 2002. Mbio hizo ni za km 5, 21 na 42.

Mhe. Waziri Mkuu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Majaliwa Kassim akizindua Mashindano ya Kili Marathon Tarehe 27.02.2022