Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania, Dayosisi ya Kaskazini ina Kitengo kinachohudumia watoto wenye ulemavu wa akili. Kitengo hicho kinaitwa Building a Caring Community (BCC).
BCC ina marafiki ambao hufanya nao kazi pamoja. Mosaic International ni mshirika mkuu na rafiki wa BCC. Wana programu inayoitwa Carman International Fellowship, ambapo kupitia programu hiyo hutuma mfanyakazi mmoja wa kujitolea kukaa na kufanya kazi pamoja na wafanyakazi wa BCC kwa kipindi cha mwaka mmoja. Fuatilia namna ambavyo Daniel Scherer- Edmund ambaye alikwepo Tanzania akifanya kazi na BCC tangu August 2022 hadi December 2023. Alifanyika baraka sana.