Msaidizi wa Askofu Mch. Deogratius Msanya kwa niaba ya Mkuu wa KKKT na Dayosisi ya Kaskazini Askofu Dkt. Fredrick Onael Shoo amemkaribisha rasmi Katibu Mkuu mpya Engr. Zebhadia Moshi alipofika ofisini kwake na katika sala ya asubuhi Ofisi Kuu DK kwa mara ya kwanza Februari Mosi, 2022.
Katika salamu zake alizotoa kwa Watumishi wa Ofisi Kuu Eng. Moshi ameomba ushirikiano akisema kila mmoja ni Katibu Mkuu katika nafasi yake na yeye ni kiongozi wao.
Anasema tunapaswa kama viongozi kuwafikisha watu tunawaongoza salama.
Engr. Moshi alichaguliwa katika kikao cha Halmashauri kuu ya 241 kilichofanyia Disemba 7, 2021 Uhuru Hotel and Conference Centre baada ya aliyekuwa Katibu Mkuu Bw. Authur Ndengerio Shoo kufariki.
Injinia Moshi alikuwa Mkurugenzi wa VETA Tanzania (Director General at Vocation Education and Training Authority)-VETA na baada ya kustaafu alijishughulisha na shughuli binafsi.