Maburudisho kwa Wachungaji Waastaafu na Wenzi wao

Wachungaji Wastaafu na Wenzi wao wamekutana kwa Maburudisho ya Siku mbili katika hoteli ya Lutheran Uhuru Hotel.

Maburudisho hayo yaliyoandaliwa na Uongozi wa KKKT Dayosisi ya Kaskazini yalikuwa na lengo la kuwakutanisha Wachungaji Wastaafu na wenzi wao ili wapate nafasi ya kushirikishana uzoefu wa maisha baada ya kustaafu, kupata ufahamu namna ya kukabiliana na magonjwa mbalimbali, kuishauri Dayosisi mambo mbalimbali kutokana na uzoefu wao katika utumishi na kuendelea kuimarishwa kiroho.
Tarehe 1-3/5/2024