MKUTANO MKUU WA IDARA YA WANAWAKE JIMBO LA KILIMANJARO MASHARIKI

Mkutano Mkuu wa Idara ya Wanawake Jimbo la Kilimanjaro Mashariki wafanyika katika Chuo cha Kilutheri cha Biblia na Theologia Mwika tarehe 29 – 30 Julai, 2021.

Neno Kuu la Mkutano huo linatoka katika Kitabu cha Nabii Isaya 55:6, “Mtafuteni BWANA, maadamu anapatikana, mwiteni, maadamu yu karibu;”.

Mkuu wa Jimbo, Mch. Calvin Koola akifungua Mkutano huo amewataka wanawake kupeleka unabii walioupokea katika sharika zao.

Kwa mujibu wa ratiba ya Mkutano, Mhe. Msaidizi wa Askofu, Mch. Deogratius Msanya, atafundisha somo la Biblia.

Taarifa ya Jimbo ya kazi za Wanawake katika Mkutano huo wa 12 inaonesha mafanikio makubwa kwa kazi za miaka miwili iliyopita.

Mkuu wa Jimbo la Kilimanjaro Mashariki, Mch. Calvin Koola akifuatilia mada katika Mkutano Mkuu wa Idara ya Wanawake.