MKUU WA KANISA AZINDUA NYUMBA YA WATUMISHI – KIMASHUKU

Mkuu wa KKKT na Mkuu wa Dayosisi ya Kaskazini, Mhe. Askofu Dkt. Fredrick Onael Shoo amezindua Nyumba ya Watumishi Usharika wa Kimashuku tarehe 4.7.2021. Aidha, Mwenyekiti wa Ujenzi, Bw. Eliezeri Ngowi, akisoma risala ya ujenzi, alitaja kuwa nyumba hiyo amegharimu kiasi cha Tzs. 132 milioni.

Msaidizi wa Askofu, Mhe. Mch. Deogratius John Msanya, akihubiri Neno la Mungu toka 2Tim. 4:1-5, ikiwa ni kilele cha mwezi wa Vijana, aliwapongeza Vijana wa Jimbo la Hai kwa kukubali kutumwa kwenda kujenga jengo la Mtaa wa Yamnono.

Alionya kuwa yanahitajika maandalizi ya kutosha kwa vijana ili kuwepo ufanisi wanapotumwa kutenda kazi hasa ya misioni na uinjilisti. Amewataka wazazi na walezi kuwapa watoto malezi ya kikristo jinsi Timotheo ulivyopata malezi ya imani toka kwa Bibi na Mama.

Pia alisema ni wajibu wa Kanisa kutoa malezi sahihi ya imani na uchaji wa ibada kwa Vijana ili kuwa na kanisa imara. Amewapongeza watumishi wa Injili kwa kuandaa Semina kwa Vijana. Vijana wanapaswa kuzitambua changamoto za sasa na kuzikabili ipasavyo kwa njia ya maombi, kuwa na bidii katika kusoma, kujifunza na kufundisha neno la Mungu kwa usahihi.

Katika ibada hiyo, Mjane wa aliyekuwa Katibu Mkuu wa Dayosisi ya Kaskazini, Bibi Arthur Ndengerio Shoo, akiwa na familia yake, walitao shukrani kwa Mungu kwa zawadi ya maisha na kazi aliyofanya mpendwa wao, Bw.   Arthur Ndengerio Shoo.

Mkuu wa Kanisa na ASkofu wa KKKT DK, Askofu Dkt. F. Shoo akifungua nyumba ya Watumishi Usharika wa Kimashuku Julai 4,2021