Salam za Pasaka za Mkuu wa Kanisa

Mkuu wa KKKT na Dayosisi ya Kaskazini Askofu Dkt. Fredrick Onael Shoo ametoa salam za Pasaka kwa Wakristo na jamii kwa ujumla Aprili  16, 2022 mjini Moshi.

Katika saalamu hizo alianza kwa kusema ni kwa Neema ya Mungu tumejaliwa kuwa na sikukuu nyingine katika mwaka huu.  Anasema tukitazama nyuma tunaona tumepita katika mambo magumu ya hatari lakini Mungu kwa Neema yake ametuwezesha kuiona na kuisherekea pasaka ya Mwaka huu hivyo ni jambo la muhimu kuungana pamoja kumshukuru Mungu.

Anasema Sikukuu ya Pasaka ndiyo sikukuu kubwa ya muhimu na ya maana kuliko nyingine zote katika historia yetu kama wakristo kwa sababu ni katika pasaka tunaadhimisha kifo cha mwokozi wetu na ufufuo wake.

 Anase mambo hayo mawili kifo na ufufuo wake ndipo kulipo na msingi wa Imani na Tumaini letu. Mateso ya Yesu Kifo chake pale Msalabani vinatufunulia upendo wa Mungu, Mungu ametupenda sisi wenye dhambi kiasi cha kumtuma mwana wake wa Pekee aje atulipie deni letu la dhambi.

Anasema kupitia damu yake iliyomwagika pale msalabani tumepata kuhesabiwa haki na kuwekwa huru.

Askof Shoo anasema katika salam zake kuwa, katika kufahamu upendo wa Yesu pia tunapaswa kujifunza unyenyekevu wa Yesu usio na kipimo wa yeye kuyaacha yote katika enzi yake kule mbinguni ashuke akubali kutiwa katika mikono ya wandamu, kuteswa na hata kuuwawa.

“Maandiko Matakatifu yanatuambia tuwe na nia hiyo hiyo kama ilivyokuwa ndani ya Yesu Kristo kwamba pamoja na kuwa na yote haya, aliuacha utukufu wake akajinyenyekesha sana hata mauti, mauti ya Msalaba, mauti ya aibu kwaajili yetu” Alisema Dkt. Shoo katika salam hizo.

Alihoji katiaka hilo tunajifunza nini sisi watumishi wa Mungu katika Unyenyekevu? Ansema Mungu ametukabidhi kundi lake kulilisha na kulitunza, Je? Tunaangalia tu mambo yetu binafsi na faida zetu binafsi tukijifanya mabwana juu ya kundi hili? Au tunalitunza kweli kwa upendo na unyenyekevu kama alivyotuonyesha Yesu?

Ametoa wito kwa watumishi wa Mungu na wote waliopewa mamlaka na madaraka kufanya nakuwahudumia watu wa Mungu kwa Upendo na unyenyekevu mkubwa tukitambua watu hawa ni wa Mungu na sisi tumepewa utumishi, madaraka na mamlaka kama dhamana tu. “Tuwatumikie kwa upendo na unyenyekevu mkubwa kama alivyotufundisha Bwana Yesu”Alisistiza Askofu Shoo.

Aidha alisema kwa kutambua jambo kubwa Mungu alilotufanyia wanadamu kupitia Mwana wake wa pekee tunapaswa kuishi Maisha ya Shukrani kwa Mungu na maisha  ya mfano kama kusameheana kama sisi tulivyosamehewa dhambi zetu.

Alihitimisha kwa kusema Pasaka hii ikatufundishe mambo ya unyenyekevu, mambo ya upendo wa sisi kwa sisi kwa maana Mungu ametupenda na hata pale tulipo koseana tusameheane.

“Tumwombe Yesu atujaze hofu ya Mungu ndani yetu, tumwogope Mungu, tumpende Mungu, Tumtii Mungu, tuwapende wanadamu wenzeutu, tuwaheshimu wanadamu wenzetu, tutenda haki, tusimame katika kweli ya Neno la Mungu, haya tukiyasimamia ndipo amani itakuwepo  na Baraka za Mungu zitakuwepo”