Tuwatembelee Wahitaji

Katibu wa Idara ya Diakonia ya KKKT Dayosisi ya Kaskazini Mch  Julius Lema ametembelea watoto wanaoshi katika mazingira magumu katika hosteli ya Usharika wa Kimashuku jimbo la Hai na kugawa msaada wa chakula Novemba 6, 2021. Watoto hao wanasoma katika shule ya msingi na sekondari Rafiki Foundation na wanafadhiliwa na sharika za Jimbo la Hai.

Sista Abema Ibrahimu mlezi wa watoto hao alimshukuru Mch. Lema na marafiki zake kwa kuwatembelea na kwa msaada waliotoa. “Tunawashukuru kwa moyo wa upendo, mmetumia muda wenu na mali zenu kuja kuwatembele watoto hawa na kuwapa zawadi, asanteni sana kwa moyo wa upendo Mungu awabariki”Alisema sista Abema.