UFUNGUZI WA JUMA LA PENTEKOSTE KKKT USHARIKA WA TARAKEA

Watumishi wa Mungu wametakiwa kulitangaza neno la Mungu kwa ufasaha ikiwa ni pamoja na kuwafundisha watu yaliyo kweli ili wasitangetange na kuanguka katika mikono ya wanyanganyi. Wito huo umetolewa na Msaidizi wa Askofu Dayosisi ya Kaskazini Deogratius Msanya wakati alipokuwa akifungua juma la pentekoste iliyofanyika KKKT Jimbo la Kilimanjaro Mashariki, Usharika wa Tarakea wilaya ya Rombo Mkoani Kilimanjaro.

Amesema kuwa Mungu wa Mbinguni anataka watu wote waokolewe na kuokolewa kwao ni kwa njia ya mafundisho na kwa  kupata habari njema za Yesu ambazo zitawatoa gizani na kuwaweka nuruni.Sambamba na hayo amesema katika juma la pentekoste ni vyema watumishi wakamuomba Roho Mtakatifu akapate kuwashukia ili kuhubiri kwao kusiwe katika hekima ya kibinadamu bali katika Nguvu za Roho Mtakatifu.

Tukishiriki watu wamuome Mungu, wasitusifie kwamba tumesoma falsafa  maana falsafa haiwezi kuwasaidia watu ,bali wauone utukufu wa Mungu kupitia mahubiri yetu yaliyojaa nguvu za Mungu “Alisema Msanya.

Amesema kuwa hayo yatawezekena kwa kadri watakavyonyenyekea na kumuomba Mungu awavike  uweza utokao juu  ili watu wamuome yeye kupitia jumbe zenye nguvu watakazo hubiri.

Jumbe zenye Nguvu simanishi kupayuka sana ,unaweza ukapayuka sana lakini ukahubiri ujumbe mkavu ,kwa hiyo tukizungumza jumbe zenye Nguvu ni uvuvio wa Roho wake tunaeaminishwa kushuka kwake atakavyotupa Nguvu na watu wamuome kupitia ujumbe huo

Hata hivyo amewataka wachungaji wainjilisti na wapuliza tarumbeta kuenenda katika Nguvu hiyo ya kushuka kwake naye akatuvuvie ili kupitia huduma watu wakaaokolewe na wapate kujua yaliyo kweli.Kwa upande wa wachungaji wamesema kuwa juma hilo la pentekoste ambayo ni kushuka kwa Yesu Kristo wamesema watalihubiri neno kwa watu wote ili mabadiliko yaweze kutokea kwa ambao hawamjui Kristo wakapate kumfahamu.