Wanavikundi UCB Wapata mafunzo Usawa wa Kijinsia na ushiriki katika Vikundi

Uchumi commercial Bank (UCB) imetoa  mafunzo kwa wanachama wake waliopo kwenye vikundi vilivyojiunga na Uchumi bank. Mmoja wa Afisa Maskoko wa Benki hiyo Bw. Elihuruma Nkini amesema wanatoa darasa la majadiliano kuhusu usawa wa kijinsia na kushirikiana katika vikundi. Semina hiyo ilifanyika katika Ukumbi wa Kristo Mfalme Moshi Kilimanjaro Julai 6, 2023 ambayo ni endelevu.

Bwana Nkini amewaeleza wanavikundi kushiriki  kikamilifu katika vikundi vyao bila kujali jinsia na kuepuka kukaa muda mrefu bila kutumia akaunti zao jambo linaloweza kusababisha akaunti zao kufungiwa kwa muda.

 “kukaa kwa kipindi cha miezi mitano bila kuweka au kutoa fedha kwenye akaunti kunasababisha akaunti kufungiwa kwa muda. Niwasii mtumie akaunti zenu vizuri, msikusanye hela na kutumia hapo kwa hapo, wekeni akiba”. Alisema Nkini

Kwa upande wa wanavikundi kuhusu usawa katika ushiriki wa masuala ya shughuli za kiuchumi; Bwana Godwin Kakuru alisema kila mtu ana haki sawa ya kushiri hivyo wanapaswa kudumisha utamaduni wa haki kwa mujibu wa sheria zetu ili waweze kuleta maendeleo kwenye vikundi na jamii kwa ujumla.

Alisema vikundi hivyo na mafunzo hayo wanayopewa yamewapa elimu inayowasaidia kukopa na kufanya shughuli za maendeleo kama  kusomesha, kujenga, kufungua biashara  nk.

Awali aliishukuru Benki ya UCB na shirika la  We Effect kwa semina wanayotoa kuhusu usawa wa kijinsia. Anasema wameelewa maana ya mikopo na inaonekana mwanamke kwa sasa anapata fursa nyingi kuliko mwanaume.

Amewataka wanaume kujitokeza na kuinuka kwa pamoja maana wanaume mawekuwa nyuma japo nao wanahitaji kusaidiwa/kuwezeshwa.

Aidha Jackline Zakayo wanakikundi alisema hapo awali wanaume wengi walizarau vikundi wakidhani kuwa vikundi ni kwa wakinamama pekee laikini kwa sasa wameelimika.