Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania KKKT anayemaliza muda wake Askofu Dkt.. Fredrick Onael Shoo Semptemba 23,2023 amekabidhiwa zawadi ya gari jipya aina ya Landcruiser ya Mwaka 2023 mpya kabisa 0 km iliyonunuliwa kiwandani.
Hii ni ahadi iliyoanza kufanyiwa kazi baada ya mmoja wa waumini wa KKKT Bw. Noah Kadiva kutoa wazo hilo kanisani Kondeni Matala Kilimanjaro katika ibada ya shukrani ya Mchungaji Eliona Kimaro April, 23 2023.
Baada ya wazo hilo ambalo lilipokelewa kwa mwitikio mkubwa iliundwa kamati ya zaidi ya watu 60 wakiwemo Wabunge, Wanasiasa, Wafanyabiashara na Waumini wa madhehebu mbalimbali wakiwemo wa KKKT na hatimaye Dkt. Shoo amekabidhiwa zawadi hiyo nyumbani kwake Mailisita, Moshi Mkoani Kilimanjaro.