Uenezaji wa Mpango Mkakati wa miaka 5 (2024-2028)

KKKT Dayosisi ya Kaskazini ipo katika utaratibu wa uenezaji wa Mpango Mkakati wa miaka 5 ( 2024-2028). Waganga wakuu wa hospitali,Makatibu wa hospitali,Wakuu wa shule za msingi na sekondari, Wakuu wa Vyuo vya ufundi pamoja na Wahasibu wao, wamepata kujengewa uwezo wa jinsi ya kuutumia Mpango Kazi huo ili kufikia malengo husika ambayo Kanisa limejiwekea kwa kipindi cha miaka 5.
Elimu hiyo imetolewa tarehe 24-25 Aprili 2024 katika ukumbi wa mikutano uliopo katika Ofisi kuu ya Dayosisi.