Huduma ya Udiakonia Magadini

Katibu wa Idara ya udiakonia Mch. Julias Lema na mtaalamu wa mazoeizi ya viungo(Physiotherapist) toka The Moshi Epignosis Physiotherapy Clinic Bw. Shedrack Domingo wametembelea familia ya Mama Christine Shenkway (63), Bw. Stanley Robson (76), na mama Marium Lepuko (66) wa Korongo Magadini wenye watoto wenye ulemavu wa viungo Oktoba 26, 2021.

Ziara hiyo ililenga kugawa msaada wa viti mwendo familia hizo kuwasaidia watoto hao wenye ulemavu waweze kutoka eneo moja hadi lingine na pia kuweza kujifanyia shughuli zao ndogondogo za maendeleo.

Mch. Lema anasema katika nyumba walizotembela mama Chistina ana watoto 4 wenye ulemavu ambapo alibaini kuwa anajukumu na uhitaji mkubwa kutokana na kutelekezwa na mume wake na kumwachia watoto hao ambao hawawezi kujisogeza na wanamtegemea kwa kila kitu.

Mch. Lema aligawa viti mwendo hivyo ili viwasaidie kujikimu na kumpa nafasi mama yao kutoka kutafuta riziki.