ASKOFU DKT. SHOO: MWENYEKITI WA 10 CCT

Askofu Dkt. Fredrick Onael Shoo Mkuu wa KKKT na Mkuu wa Dayosisi ya Kaskazini, amechaguliwa kuwa mwenyekiti wa Jumui ya Kikristo Tanzania (CCT) kwenye Mkutano Mkuu wa 31 wa Jumuiya hiyo uliofanyika mkoani Morogoro kwenye Kituo cha Mafunzo ya Wanawake cha CCT tarehe 08-09 Julai 2021.

Katika uchaguzi huo Askofu Shoo alichaguliwa kwa kura 63 kati ya kura 212 zilizopigwa na kuwashinda wagombea wenzake Askofu Stanley Hotay wa Kanisa la Anglican Dayosisi ya Mount Kilimanjaro aliyepata kura 50, aliyekuwa mwenyekiti Askofu Dkt. Alinikisya Cheyo wa Kanisa la Morvian Tanzania aliyepata kura 47.

Wengine ni Askofu Dkt. Mahimbo Mndolwa Mkuu wa Kanisa la Anglikana kura 29, Askofu Mussa Mwageswele wa Kanisa la Afrikan Inland Church Tanzania (AICT)kura 23.

Baada ya uchaguzi wa Mwenyekiti, Askofu Stanley Hotay wa Kanisa la Anglikana Dayosisi ya Mount Kilimanjaro alichaguliwa kuwa Makamu mwenyekiti wa Kwanza kwa kupata kura 86, akifuatiwa na Askofu Dkt. Cheyo kura 62, Dkt. Mndolwa kura 40 na Askofu Mwageselwa kura 22.

Makamu wa pili wa mwenyekiti alichaguliwa Askofu Dkt. Cheyo aliyepata kura 84 akimshinda Askofu Dkt. Mndolwa aliyepata  kura 66 na Askofu Mwageselwa kura 57.