Baba Askofu Dkt Frederick Onael Shoo azindua Mahoma Parish House.

Jengo Hilo limejengwa kuanzia 2018 na kukamilishwa ndani ya miaka 5. Aidha, lilikisiwa kujengwa kwa Tzs. Milioni 500M na mpaka kukamilika limetumia takribani 458M. Lina Ofisi ya Usharika, Kindergarten, Ukumbi wa Mkutano, Vyumba vya Wageni, Huduma za Fedha na Duka Agosti 14, 2022.

Akihubiri Neno la Mungu kutoka 1Kor. 1: 26-31 katika Ibada alifundisha kwamba hekima ya Mungu ni tofauti na ya Dunia hii. Kama vile Mungu ametumia vinyonge kudhihirisha nguvu zake. Hekima ituingizayo mbinguni ni Yesu Kristo mwenyewe.

Hekima ya Dunia hii inatuweka mbali na njia ituingizayo mbinguni na inaleta uharibifu hata katika ndoa ya kikristo. Inasema moyoni hakuna Mungu. Inadharau uwepo wa Mungu. Inaudharua msalaba na nguvu yake ya wokovu. Inaona mambo yote ya kimungu ni upuuzi. Inakataa kutenda mapenzi na maagizo ya Mungu. Inatasahaulisha kuwa maisha hata ni mafupi. Inasahaulisha hukumu ya Mungu. Haimhitaji Yesu. Wasio na Yesu hawana raha moyoni.

Yesu ndiye hekima ya Mungu ituingizayo mbinguni. Hata katika maisha ya ndoa tunamhitaji Yesu awepo ili pawepo amani, furaha, utulivu, na baraka. Tushike Yesu peke yake katika safari ya hapa duniani.

Hekima ya Mungu inatufundiaha kuwa watendaji wa Neno na sio tu wasikiaji wa Neno. Kadhalika ndoa zetu ziwe katika msingi imara wa Neno la Mungu. Mahali ambapo mapenzi ya Mungu yanatimizwa.