Mkutano Mkuu wa 15 wafanyika Hai

Jimbo la Hai la Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania Dayosisi ya Kaskazini, limefanya Mkutano wake Mkuu wa 15 Oktoba 14, 2021 katika viwanja vya vya jimbo hilo ambapo taarifa ya jimbo hutolewa na Mkuu wa Jimbo na kujadiliwa na wajumbe toka sharika zote za Jimbo kisha kuweka maazimio na mipango mbalimbali ya jimbo.

Mkutano huu hufanyika kila baada ya miaka miwili kwa mujibu wa Katiba ya Dayosisi ya Kaskazini ambacho ndicho chombo muhimu kinachotoa fursa ya kufanya tathimini ya utekelezaji wa mipango ya jimbo kwa miaka miwili iliyopita na kuweka mipango itakayofanyika katika kipindi kingine cha miaka miwili.

Mkuu wa Jimbo la Hai Mch. Malya alitoa taarifa utekelezaji ya miango na maendeleo ya miaka miwili ambayo baada ya taarifa hiyo wajumbe waliijadili na kisha kutoa maazimio ya pamoja.

Mhe. Msaidizi wa Askofu Mch. Deogratius Msanya alitoa neno la ufunguzi kwa niaba ya Mhe. Baba Askofu Dkt. Fredrick Shoo. Awali  alimshukuru Mungu kwa kupigania masisha ya mwanadamu wakati wote na kupongeza Jimbo  kwa maandalizi mazuri ya mkutano huo.

Aliwataka watu kuwa na mioyo inayomtazama Mungu, kumwelekea Mungu  na kumtumikia kila mmoja kwa nafasi yake “Mungu anatuambia katika ujumbe huu kutoka kwa Nabii Ezekieli kuwa, kila mmoja kwa nafasi yake tumeitwa kuwa watumishi wa Mungu, uwe mkristo raia au wale waliotengwa kumtumikia Mungu” Alisema Mchungaji Msanya.
Pia aliwaasa Wakristo kujihadhai na  mtego wa kuwa na kiburi na kujihesabia haki. Alisema tumeitwa kuwa watumishi kwa Neema ya Mungu tu na si kwa kustahili kwetu
Neno kuu lilitoka katika kitabu cha Ezekiel 11 19 “Nami nitawapa moyo mmoja name nitatia roho mpya ndani yao; name nitaondoa moyo wa jiwe katika miili yao, name nitawapa moyo wanyama”