UPANDAJI MITI AGAPE

Mhe. Baba Askofu Dkt. Frederick Onael Shoo, Mkuu wa KKKT na Mkuu wa Dayosisi ya Kaskazini ameongoza zoezi la upandaji miti katika Seminari ya  Agape ya KKKT Dayosisi ya Kaskazini Aprili 27, 2021. 

Zoezi hilo lilienda sambamba na uzinduzi wa msitu tengefu ambapo wanatarajia kupanda miti elfu 50. 

Mkuu wa Seminari hiyo Mch.  Godrich Lyimo amesema kwa sasa wameshaotesha miti zaidi ya elfu 15, lengo ni kuotesha miti elfu 50. Alisema ni desturi kwa kila mwanafunzi kupanda mti na kuutunza pindi anapowasili shuleni hapo.

Mtafiti wa masuala ya mimea kutoka chuo kikuu cha Bayreuth nchini Ujerumani Andreus Hemp, ameahidi kuanzisha kitalu kikubwa cha miti katika Sekondari hiyo, kuhakikisha suala la upandaji na uhifadhi wa mazingira linakuwa  endelevu.

Dkt. Andreas amesema wanajitahidi kurejesha hali ya uoto wa asili kwa maisha ya viumbe na binadamu.

Askofu Dkt. Fredrick Shoo mwenye shati la zambarau na msaidizi wake Mch. Deogratius Msanya mwenye shati la kijivu pamoja na wadau wa mazingira, walimu na wanafunzi wa Agape sekondari baada ya upandaji miti.