ASKOFU SHOO AWEKA WAKFU NYUMBA YA IBADA YA USHARIKA WA TPC NA MITAA YAKE

Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania na Mkuu wa Dayosisi ya Kaskazini Askofu Dkt. Fredrick Shoo amewataka wakristo kulisoma neno la Mungu pamoja na kuliamini ili neema ya Mungu ikapate kuambatana na maisha yao.

Askofu Shoo ameyasema hayo wakati alipokuwa akiweka wakfu nyumba ya ibada ya  Usharika wa Tpc na Mitaa yake miwili ambayo ni mtaa wa Mandila na mtaa wa Makumbusho iliyofanyika Jimbo la Kilimanjaro Kati Mkoani kilimanjaro.

Amesema kuwa siku hizi watu hawana kiu wala njaa juu ya mambo yanayomuhusu Mungu na kusema wameamua kujishibisha  roho zao kwa mambo mengine .

Amesema kuwa katika maandiko Yesu mwenyewe anasema kila aonaye kiu na aje nakusema atakayekwenda kwake atampatia kile ambacho hakiwezi kupatikana  sehemu yeyote .

 Sambamba na hayo amesema kuwa, wakristo wa sasa wamekuwa hawajishughulishi katika kulisoma neno la Mungu bali wamekuwa  wakihangaika kwa watu wasio sahihi pamoja na  kutoa mali nyingi kwa ili wafanikiwe jambo ambalo vitu vyote hivyo vinatolewa bure na Yesu mwenyewe.

Amesema kuwa wana wa Izraeli wakati ule walipokuwa kule utumwani  Babeli walikuwa na mahangaiko na shida mbalimbali na walikuwa wamepoteza matunaini lakini Mungu aliwaandaa ili kuwarudisha katika nchi ya ahadi.

“Leo tumeimba Njooni kwa mponya  njoo sasa  Mungu ameweka mwaliko wake kwa watu ili watu waje kwake wamrudie yeye ili wapate kuponywa,Mungu akamalize kiu zao. Kiu tunaweza kusema ni shida mbalimbali,mahangaiko na ukiangalia hata leo watu wako kwenye mahangaiko ya kila namna,  watu hawajatulia ndani ya mioyo yao ,Mungu anakuwambia wewe Sasa hivi kama unaona kiu uje kwake na naye atakupa maji na chakula cha kukushibisha.”Alisema Shoo.

Mchungaji kiongozi wa Usharika huo wa Tpc David Pallangyo amesema kuwa Usharika huo una Mitaa minne ambayo ni Mandila, Mserekia, Makumbusho, Masini na Mtaa wa Kati.

Amesema kuwa jengo la mtaa wa Makumbusho limefanyiwa ukarabati tangu Januari na imegharimu kiasi cha shilingi milioni kumi na tano  mpaka kumalizika.

Hata hivyo amesema kuwa jengo hilo la ibaada la Usharika  wa Tpc imegharimu kiasi Cha shilingi milioni 96 mpaka kukamilika  na kusema Usharika huo wa TPC umeshiriki kazi mbalimbali za Kanisa  zinazohusu  Jimbo , Dayosisi na kwa ujumla

Hata hivyo waumini walioshiriki katika uzinduzi wa huo wameeleza furaha yao na kusema kuwa wanamshukuru Mungu kwa kuwawezesha kumaliza nyumba hiyo ya ibada .

Msharika wa Usharika wa Tpc amesema kuwa wanatoa shukrani nyingi kwa watu wote walioshiriki kwa namna moja au nyingine katika ukarabati wa jengo hilo la ibada hadi kukamilika.