Benki ya Uchumi Commercial Yawafunda Mawakala

Benki ya Uchumi Commercial (UCB), imetoa semina kwa mawakala wake ikiwa ni mpango wa benki hiyo kuwajengea uwezo mawakala kutoa huduma bora kwa wateja na kutekeleza takwa la Benki kuu ya Tanzania; Semina hiyo imefanyika mwanzoni mwa mwezi Machi, 2024 Umoja Lutheran Hotel Mjini Moshi.

Akizungumza wakati wa ufunguzi wa semina hiyo, mkuu wa idara ya maendeleo ya masoko wa Uchumi Commercial Bank (UCB) Bw. Israel Lyatuu alisema dhumuni la semina hiyo ni pamoja na kuwajengea uwezo mawakala kuweza kutoa huduma bora kwa wateja, kutimiza takwa la kisheria kwa mujibu wa Sheria za Benki Kuu ya Tanzania la kuwajengea mawakala uwezo, mawakala kuijua zaidi uchumi benki na kufahamiana.

” Leo ukiachana na kutimiza Sheria ya benki kuu tumelenga kutoa elimu kuhusu utoaji wa huduma bora kwa wateja, namna ya kubaini na kupambana na vitendo vya utakatishaji wa fedha, Sheria za mawakala na kufahamiana.

Niwaombe mawakala kuwa wasikivu, na kushiriki kikamilifu katika warsha hii”. Alisema Lyatuu.

Bw. Israel alisema huduma za Benki ya Uchumi kwa mawakala ilianza mwaka 2018 na wana jmla ya mawakala 73 hadi sasa.

Baadhi ya mawakala wa UCB kwenye semina Umoja Lutheran Hotel