Category: Dayosisi

Askofu Dkt. F. Shoo Achaguliwa tena Miaka Sita

Mkutano mkuu wa KKKT Dayosisi ya Kaskazini uliofanyika tarehe 30.08.2024, umemwomba Askofu Dkt. Fredrick Shoo, kuendelea na nafasi ya Mkuu wa Dayosisi ya Kaskazini kwa miaka mingine sita. Mkutano huo pia umemchagua tena Msaidizi wa Askofu Mch. Msanya kwa kura na kupita kwa zaidi ya asilimia 97, kuendelea na nafasi yake kwa miaka mingine minne. […]

Read More

Kuwahudumia Watu Wenye Mahitaji Maalumu ni Wajibu wa Kanisa

Askofu Dkt. Fredrick Onael Shoo Mkuu wa KKKT Dayosisi ya Kaskazini amesema, suala la kuwasaidia na kuwahudumia watu wenye mahitaji maalumu ni wajibu wa Kanisa. Askofu Shoo, aliyasema hayo alipokuwa akigawa viti mwendo kwa watoto wenye ulemavu wa viungo Jimbo la Karatu. Jumla ya viti mwendo 24 vyenye thamani ya zaidi ya Shilingi Milioni 1.5 viligawanywa […]

Read More

Konde Yatembelea Dayosisi ya Kaskazini

Jopo la Wachungaji 18 wa KKKT Dayosisi ya Konde Jimbo la Mbeya Magharibi wametembelea KKKT Dayosisi ya Kaskazini. Katika ziara hiyo iliyoongozwa na Mkuu wa Jimbo la Mbeya Magharibi Mch. Lusajano Sanga ililenga kuimarisha ushirikiano wa Dayosisi hizi mbili pamoja na kujifunza mambo mbalimbali yanayofanyika katika Dayosisi ya Kaskazini. Hata hivyo walipata fursa ya kujifunza […]

Read More

MCH. MSANYA “KANISA LINA WAJIBU WA KUTOA ELIMU YA AFYA….

Msaidizi wa Askofu KKKT Dayosisi ya Kaskazini Mch. Deogratius Msanya amesema kuwa, Kanisa lina wajibu wa kutoa elimu  ya afya ili kuhakikisha kuwa washarika wanajikinga na magonjwa mbalimbali hususani magonjwa yasiyo yakuambukiza. Aliyasema hayo wakati akihitimisha maadhimisho ya wiki ya afya ya msingi, kidayosisi yaliyofanyika jimbo la Karatu Usharika wa Endalah Julai 14, 2024. Alisema […]

Read More

Mkurugezi TAMISEMI: Kongole KKKT kwa kuwahudumia Walemavu.

Mkurugenzi wa huduma za jamii ofisi ya Rais TAMISEMI, anayeshughulikia masuala ya watu wenye ulemavu Bi. Amina Faki, amelipongeza Kanisa kwa jitihada kubwa inayoifanya ya kuwahudumia watoto wenye ulemavu wa akili pamoja na makundi  mbalimbali ya watu wenye uhitaji maalumu.. Bi. Faki ametoa pongezi hizo kwenye bonanza la michezo la watoto wenye ulemavu wa akili […]

Read More

TUWEKEZE KWA WATOTO NA VIJANA KWA KUWAFUNDISHA MAADILI MEMA

Mkuu wa KKKT  Dayosisi ya Kaskazini Askofu Dkt. Frederick Onael Shoo, amesema ni vyema  Kanisa likahakikisha  kuwa waalimu wanaowafundisha watoto vipindi vya dini Makanisani waandaliwe vizuri ili wawafundishe misingi imara itakayowasaidia katika maisha yao ya sasa  na ya baadaye. Askofu Shoo aliyasema hayo kwenye ibada ya uzinduzi wa usharika mpya wa Pumuwani, jengo la ibada […]

Read More

Siku ya Bwana ya Pentekoste – Usharika wa Karatu mjini

Neno kuu  katika ibada hiyo lilikuwa “Roho Mtakatifu Nguvu Yetu” Ibada ya Siku ya Bwana ya Pentekoste ilifanyika katika kanisa la KKKT Dayosisi ya Kaskazini Usharika wa Karatu mjini. Ibada hii ni pamoja na hitimisho la maadhimisho ya Juma la Pentekoste ambalo kidayosisi imeadhimishwa katika Jimbo la Karatu. Mheshimiwa Baba Askofu Dkt. Fredrick Shoo aliongoza […]

Read More

JUMA LA PENTEKOSTE- KARATU

Juma la Pentekoste lafunguliwa Karatu, zaidi ya wahubiri 164 na wapiga tarumbeta 80 washiriki! Msaidizi wa Askofu wa KKKT Dayosisi ya Kaskazini Mch. Deogratius Msanya, ameongoza ibada ya ufunguzi wa Juma la Pentekoste Usharika wa Karatu Mjini Mei 11, 2024.Juma hilo Kidayosisi linafanyikia katika Jimbo la Karatu kuanzia Mei 11 – 19, 2024. Msaidizi wa […]

Read More

Maburudisho kwa Wachungaji Waastaafu na Wenzi wao

Wachungaji Wastaafu na Wenzi wao wamekutana kwa Maburudisho ya Siku mbili katika hoteli ya Lutheran Uhuru Hotel. Maburudisho hayo yaliyoandaliwa na Uongozi wa KKKT Dayosisi ya Kaskazini yalikuwa na lengo la kuwakutanisha Wachungaji Wastaafu na wenzi wao ili wapate nafasi ya kushirikishana uzoefu wa maisha baada ya kustaafu, kupata ufahamu namna ya kukabiliana na magonjwa […]

Read More

Uenezaji wa Mpango Mkakati wa miaka 5 (2024-2028)

KKKT Dayosisi ya Kaskazini ipo katika utaratibu wa uenezaji wa Mpango Mkakati wa miaka 5 ( 2024-2028). Waganga wakuu wa hospitali,Makatibu wa hospitali,Wakuu wa shule za msingi na sekondari, Wakuu wa Vyuo vya ufundi pamoja na Wahasibu wao, wamepata kujengewa uwezo wa jinsi ya kuutumia Mpango Kazi huo ili kufikia malengo husika ambayo Kanisa limejiwekea […]

Read More